DSE Price Updates

                              TOL 330.00     TBL 1,800.00     TTP 510.00     TCC 1,640.00     SIMBA 1,780.00     SWISSPORT 650.00     TWIGA 1,340.00 -20.00     NICOL 305.00     DCB 360.00     KA 1,500.00     EABL 2,000.00     JHL 5,860.00    
LAST UPDATE: 24/9/2008 - 5:58PM EAT

Thursday, September 4, 2008

Private tax collection system likely to reduce corrupt elements

2008-09-04 11:10:20
By Angel Navuri


Private tax collection is likely to reduce corruption at the collection point by offering mechanisms for penalising poor collectors, a recent study by Research on Poverty Alleviation (REPOA) has revealed.

According to the study, a private tax collector has in general a stronger personal interest in collection results and is prone to employ more effective mechanisms for penalising poor performance on the part of the collector. More...


[SOURCE: THE GUARDIAN]


What are your views on this? Will a private tax collection system be truly able reduce corruption which we all know exists plentifully in TRA? Or will this move just be another opportunity for 'Mafisadi' to make some extra cents? What have we been reduced to, as a country, if even something as vital as taxation has to be done by private agencies?

1 comment:

Anonymous said...

Ukiangalia report ya REPOA iligusa sana Local Government.
Makusanyo ya kodi kwa serikali za mitaa ni tofauti na serikali kuu, katika dhana ya nani ni mkusanyaji. Kwa serikali kuu makusanyo hufanywa na TRA na kwa serikali za mitaa,halmashauri nyingi sasa za wilaya, mji, mji mdogo au jiji zimetoa tenda kwa mashirika au makampuni ya watu binafsi ili kuwakusanyia kodi.

Njia ya makampuni binafsi inaonekana kuleta makusanyo mengi kuliko yalivyokuwa yakiletwa na wafanyakazi wa halmashauri hizo husika lakini tatizo lake ni pale wahasibu wa halmashauri hizo wanapopanga au kukadiria makusanyo kwa kiwango kidogo kuliko hali halisi ilivyo. Kwa njia hii wao hushirikiana na hayo makampuni na kuwezesha makampuni hayo kukusanya kodi ya ziada na kuripoti kiasi fulani zaidi ya kile kilichopangwa ili kuonesha mafanikio. Lakini ukweli ni kwamba kiwango kikubwa kilipatikana na kugawana wao na mhasibu mkuu wa wilaya, mji au jiji na timu yake ya walaji kama madiwani, makatibu kata, wakurugenzi wa hizo halmashauri na hata wakuu wa wilaya husika. kwa njia hii huwa wanaendeleza rushwa isiyo ya wazi, ambayo ilikuwepo zamani ya wafanyakazi wadogo wadogo waliokuwa wakionekana kuchukua rushwa wazi wazi na kubakiza rushwa ya wataalamu wachache.

TRA-(Tanzania Revenue Authority) pia inabidi ifanye utaratibu kama huu kwa serikali kuu, lakini sasa inakuwa ngumu, kwa kuwa serikali kuu haina njia ya kuwabana hata wataalamu wake wa ushuru, kodi na ukadiriaji mapato katika kuzuia wizi au rushwa hiyo.
Mfano ,mzuri wa ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mashirika binafsi upo huko Marekani. Pamoja na kwamba IRS- (Internal Revenue Service) ndio msimamizi na mpanga sera, sheria na mkusanyaji mkubwa wa mapato na kodi ya serikali ya Marekani chini ya wizara yake ya fedha. Lakini bado kwa kiwango fulani kikubwa kabisa na cha kushangaza imeacha utaratibu mzima wa ukusanyaji wa kodi kwa mashirika binafsi, kwa mfano :
1. H&R Block, kila mwisho wa mwaka kwa ulinganisho na IRS hungalia na kuona kama kuna watu binafsi walilipa kwa kukatwa kodi inayotakiwa kulingana na kazi walizofanya kwa mwaka huo. Kwa mtindo huu IRS hulipa kodi ya ziada kwa wale waliolipa zaidi (Tax returns) na pia hudai zaidi kwa wale waliokatwa kidogo.
2. CPA firms na wahasibu wa mashirika na makampuni ya kati na yale makubwa , hufanya mlinganisho wa kodi, za mashirika yao au wanayoyafanyia kazi na biashara zao kupitia payroll zao na ripoti zao za fedha za kila mwaka na kuona kama walilipa kodi zilizotakiwa kulipwa na kama hawakulipa basi hudaiwa ziada
3. Pia IRS imeingia mktaba na Makampuni mengine makubwa ya kukusanya ushuru katika bandari za bahari, maziwa, mito na njia za anga nk ambazo majukumu yake ni kuhakisha kwamba ushuru wa mapato na kodi husika inatozwa na serikali kupata mapato.

Katika hali hizi zote bado IRS makao makuu na katika vituo vyake vingine husimamia ukusanyaji wa ushuru , kodi na mapato ya serikali kwa kuhakisha kwamba wanajua kwa uangalifu mkubwa nani analipa nini na nani halipi nini katika dafatari lao ushuru. Tofauti kwa hapa Tanzania ni kwamba tumecopy kiasi kidogo sana cha njia za kukusanya kodi kutoka Marekani , ambapo pamoja na kuwa na wataalamu kutoka IRS hapa TRA, bado tunatumia njia za kizamani za kukusanya mapato.
Kwa sasa utaona TRA inavuka viwango kwa kukusanya kodi kila mwaka lakini ukilinganisha na uwezo wa kukusanya kodi na ushuru bado tuko nyuma sana.
Hatuna daftari la kujua ni nani analipa nini na yuko wapi , hatuna njia au mtandao uliowazi wa kujua hilo, hatuna njia za kudumu za kuwezesha hilo. Ninachoona hapa Dat ni kila anayekuja kutoka semina Uingereza , ufaransa au ujerumani anakuja na jia yake mpya. Au wakija wataalamu wa semina kutoka huko Marekani basi tinabadili tena mamabo Fulani Fulani, au wasomi wetu wa hapa mlimani na IFM wakisema jambo Fulani basi tunabadili badili. Tunatakiwa kubadili njia za ukusanyaji na wala sio kuweka viraka kila siku katika sera na wala sio sheria.
Mianya mingi imeachwa makusudi kabisa ili rushwa , wizi, na umangi-meza uweze kuendelea.
Nilipata kuenda Marekani semina ya miezi sita na nilikuwa kituo cha Sacramento , CA. Nilijionea jinsi waMarekani walivyoweza kuunda utaratibu mahususi wa ukusanyi kodi na mapato yao kiasi kwamba kila mtu na shirika analipa kodi. Japo tulifundishwa pia kwamba kuna watu na mashirika mengi yanakwepa kodi lakini IRS bado inawajua na inawafuatilia kwa karibu huku ikipata kwa sasa kinachotakiwa kupatikana bila kukosa kabisa.
Malipo ya mshahara sasa hapa TRA ni mazuri na hivyo sababu ya wizi na rushwa sioni kama una maana. Kama tungekuwa tumeona huko nje jinsi rushwa ilivyo sumu kwa kiasi Fulani tusingeweza kuwa wezi kiasi hiki hapa Tanzania. Maana kila kijana ninayemuona hapa ofisini ana biashara za wizi na rushwa hivyo kuikosesha serikali mapato.
Ningependekeza kwa kiasi kikubwa kabisa ni bora hii kazi ikafanywa na makampuni binafsi tu na wafanyakazi wachache waliopo hapa Ofisi kuu wakawa ni wasimamizi na wapangaji wa sera, sheria na udhibiti wa kodi tu.